Tuesday, July 7, 2009

kuvunja kamati!

bwana na bibi john momadi wanapenda kuwataarifu ndugu na marafiki wote kwamba wanatarajia kuvunja kamati ya harusi yao jumapili ya tarehe 12 julai.
muda na mahali na mipango mingine mtaarifiwa siku za usoni.
kwa maelezo zaidi wasiliana na uongozi wa zakaria chuma

shukrani.

shukurani ya pekee!

Familia ya mama ana kwabu wametoa shukurani ya pekee ya mpendwa wao marehemu lewis masumbuko katika kanisa la KKKT usharika wa maneromango ambapo walishirikiana na familia ya Muhoza, baadaye walikutana kwa chakula pale Boga kwa Bibi Mbega kabla ya kurejea jijini dar.

pia kwa wale wakritso wa dhehebu kilutheri mnakumbushwa kwenda kujiandikisha katika
usharika wetu wa maneromango na kusaidia katika shughuli za maendeleo ya usharika wetu na kijiji kwa ujumla.

habari za wagonjwa

ndugu wana ukoo, tunamepokea habari za wagonjwa.
mama neema (mwamini mweleka) amelazwa katika hopistali ya temeke na pia tulipata habari za kusukmbuliwa kwa dada catherine mpapasingo pale mwenge jijini dar.
tunawapa pole wao pamoja na familia zao, bwana awatie nguvu na kuwapa afya njema.
kwa maelezo zaidi wasiliana na uongozi wa zakaria chuma au wanafamilia moja kwa moja.


asante

Friday, July 3, 2009

kujiuzuru na uongozi wa zakaria chuma

shalom,

kwa uongozi mzima pamoja na wanachama wote/wanaukoo wa zakaria chuma.

kwa masikitiko makubwa napenda kutoa taarifa fupi ya tamko la kujiuzuru kwangu kwenye ngazi ya ukatibu msaidizi wa zakaria chuma.
mengi nitayaongea tutakapokuwa na mkutano mkuu ila kwa ufupi ni kwamba nafsi yangu inawiwa kujiuzuru kutokana na kwamba sioni kwamba ninawetwendea haki wanachama wa ukoo wa zakaria chuma kwa kushindwa kwangu kutimiza malengo na mikakati tuliojiwekea kwa zaidi ya mwaka sasa tangu kuchaguliwa, bila na kuwa na sababu zenye uzito.
ni dhahiri kwamba wako wanachama wengi ambao wangeweza kulisukma gurudumu la maendeleo ya umoja huu, hivyo kwangu mimi si vema nikaendelea kuwapo kwenye safu ya uongozi kwa muda wa miaka mitatu bila kufanikisha malengo tuliyojiwekea.

asanteni,

Bwana na azidi kutubariki.

Tuesday, February 17, 2009

taarif za ndoa

tunapenda kuwapa taarifa chache zilizoufikiwa uongozi wa zakaria chuma juu ya vijana na mabinti ambao wameendelea kuukimbia ukapela na kuamua kujikita katika maisha mapya ya ndoa.
kwanza tunataaarifa ya ndoa ya dada binti Mumbi ambaye anatarajiwa kuagwa tarehe 23 Aprili 2009. Vikao vya maandalizi ya shughuli hii vimashaanza katika ukumbi wa Kilimanjaro Bar pale Mwenge kituoni. Kikao kingine kitakuwa j2 ijayo hapo hapo mwenge - kilimanjaro bar.
ndugu mnaombwa kushirikiana na familia ya Mzee Mumbi ili kuweza kufanikisha shughuli hii.

dondoo nyingine ni kwamba, Mwl. Daudi Manyerere wa Mkwawa University - Iringa naye ameshakamlisha shughuli za uchumba na mipango ya harusi yake iko kwenye mchakato. tutawaletea taarifa rasmi mwishoni mwa wiki hii.

pia kuna habari kwamba katibu wetu kaka John (Tall) Momadi naye yuko safarini moshi akiwa ameambata na Mzee wetu John Gunda kukamilisha mambo ya uchumba.

taarifa kamili za shughuli hizi zote tutaweletea mwishoni mwa wiki hii, kaa chonjo!

taarifa za wagonjwa

wapendwa wana -zakaria chuma popote mlipo duniani pamoja na wadau wengine wote, tunapenda kuwapa taarifa za wagonjwa.
kwanza tunaye mama mch. catherine kitale wa karakata dar-es-salaam, ambaye amekuwa akisumbuliwa kwa kipindi kirefu sasa na amaeendelea kupata tiba katika hospitali ya Mama Ngoma pale Mwenge.
msaada wenu wa hali na mali unahitajika sana kusaidia gharama za huduma hii.
kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na familia ya Askofu Kitale kwa simu 0712700012 ama kufika nyumbani karatata wakati wowote.
pia unaweza kuwasiliana na uongozi wa zakaria chuma

James Mumbi - M/kiti
Dr. David Mwenesano -M/M.kiti - 0755447793
John Momadi - Katibu - 0713261819
Robert Manyerere - M/Katibu 0715252540
Betty Mbega - M/Hazina
Sarah Urembo - M/M.Hazina