tunapenda kuwapa taarifa chache zilizoufikiwa uongozi wa zakaria chuma juu ya vijana na mabinti ambao wameendelea kuukimbia ukapela na kuamua kujikita katika maisha mapya ya ndoa.
kwanza tunataaarifa ya ndoa ya dada binti Mumbi ambaye anatarajiwa kuagwa tarehe 23 Aprili 2009. Vikao vya maandalizi ya shughuli hii vimashaanza katika ukumbi wa Kilimanjaro Bar pale Mwenge kituoni. Kikao kingine kitakuwa j2 ijayo hapo hapo mwenge - kilimanjaro bar.
ndugu mnaombwa kushirikiana na familia ya Mzee Mumbi ili kuweza kufanikisha shughuli hii.
dondoo nyingine ni kwamba, Mwl. Daudi Manyerere wa Mkwawa University - Iringa naye ameshakamlisha shughuli za uchumba na mipango ya harusi yake iko kwenye mchakato. tutawaletea taarifa rasmi mwishoni mwa wiki hii.
pia kuna habari kwamba katibu wetu kaka John (Tall) Momadi naye yuko safarini moshi akiwa ameambata na Mzee wetu John Gunda kukamilisha mambo ya uchumba.
taarifa kamili za shughuli hizi zote tutaweletea mwishoni mwa wiki hii, kaa chonjo!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment