Friday, July 3, 2009

kujiuzuru na uongozi wa zakaria chuma

shalom,

kwa uongozi mzima pamoja na wanachama wote/wanaukoo wa zakaria chuma.

kwa masikitiko makubwa napenda kutoa taarifa fupi ya tamko la kujiuzuru kwangu kwenye ngazi ya ukatibu msaidizi wa zakaria chuma.
mengi nitayaongea tutakapokuwa na mkutano mkuu ila kwa ufupi ni kwamba nafsi yangu inawiwa kujiuzuru kutokana na kwamba sioni kwamba ninawetwendea haki wanachama wa ukoo wa zakaria chuma kwa kushindwa kwangu kutimiza malengo na mikakati tuliojiwekea kwa zaidi ya mwaka sasa tangu kuchaguliwa, bila na kuwa na sababu zenye uzito.
ni dhahiri kwamba wako wanachama wengi ambao wangeweza kulisukma gurudumu la maendeleo ya umoja huu, hivyo kwangu mimi si vema nikaendelea kuwapo kwenye safu ya uongozi kwa muda wa miaka mitatu bila kufanikisha malengo tuliyojiwekea.

asanteni,

Bwana na azidi kutubariki.

No comments: